Luke 19:1-4

Zakayo Mtoza Ushuru

1 aIsa akaingia Yeriko, naye alikuwa anapita katikati ya huo mji. 2Tazama, palikuwa na mtu mmoja mkuu wa watoza ushuru naye alikuwa tajiri, jina lake Zakayo. 3Yeye alikuwa akijitahidi kumwona Isa ni mtu wa namna gani. Lakini kutokana na umati mkubwa wa watu hakuweza kwa sababu alikuwa mfupi wa kimo. 4 bKwa hiyo akatangulia mbio mbele ya umati wa watu akapanda juu ya mkuyu ili amwone Isa, kwa sababu angeipitia njia ile.

Copyright information for SwhKC